Wanasayansi duniani wameziomba Mamlaka za Afya barani Afrika kuchukua tahadhari dhidi ya malaria sugu ambayo inadaiwa kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kuambukizwa.

Taarifa zinasema kuwa viwango vya dawa vimeonekana kutofanya kazi katika baadhi ya maeneo kutoka chini ya asilimia 1 hadi zaidi ya asilimia 20 katika kipindi cha miaka mitatu.

Wanasayansi hao wamedai mara ya mwisho dawa kutofanyakazi dhidi ya malaria sugu barani Afrika kulisababisha ongezeko kubwa la watoto kufariki.

Jopo hili la wanasayansi lililoundwa na watu 28 kutoka nchi 10 limegundua kuwa Artemisinin huua vimelea vya malaria sugu na ndio msingi wa matibabu ya ugonjwa huo.

Wameongezea kuwa vimelea sugu kwa dawa zenye artemisinin viliibuka kwa mara ya kwanza barani Afrika nchini Rwanda, na kisha nchini Uganda na Eritrea.

Hivi sasa, zaidi ya  asilimia10% ya maambukizi ya malaria husababishwa na vimelea sugu nchini Ethiopia, Eritrea, Rwanda, Uganda na Tanzania.

“Sasa ni wakati wa kuchukua hatua kabla ya mamilioni ya watu kufariki dunia kwa sababu ya tiba za malaria zisizo na ufanisi,” alisema Prof Olugbenga Mokuolu, kutoka idara ya watoto katika Chuo Kikuu cha Ilorin nchini Nigeria.

Mnamo 2016, aina sugu ya vimelea vya malaria  sugu viligunduliwa Kaskazini mwa Uganda na kufikia 2019, zaidi ya asilimia 20 ya vimelea vilikuwa sugu katika mikoa kadhaa nchini humo.

Chanzo: BBC

Please follow and like us:
Pin Share