Afrika Kusini imepeleka wanajeshi zaidi na zana za kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa ni wiki chache tu baada ya askari wake 14 kuuawa kwenye mapigano na waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo.
Vyanzo kadhaa vya kisiasa na kidiplomasia vimesema kwamba takribani wanajeshi 700 hadi 800 wa Afrika Kusini wamepelekwa mjini Lubumbashi.
Afrika Kusini inaiunga mkono Serikali ya Congo katika mapambano dhidi ya waasi wa M23, ambao hivi sasa wanadhibiti mji wa Goma, mashariki mwa Congo, na wametishia kukamata maeneo mengine muhimu.
Hii inajiri huku hali ya utulivu ikiripotiwa kwa siku ya pili mfululizo mashariki mwa Congo, baada ya wiki kadhaa za mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-32-1024x448.png)