Safari ya Afrika katika kushiriki michuano ya kombe la dunia imekuwa ya milima na mabonde, lakini sasa Afrika inaelekea kuvunja ilichopanda kwa dalili zilizopo.

Mwaka 1966 katika fainali za kombe la dunia zilizofanyikia nchini Uingereza na wenyeji kuwa mabingwa, Bara la Afrika halikuwa na mwakilishi katika michuano hiyo kutokana na upendeleo wa wazi kwa nchi za Ulaya na Marekani kupewa nafasi nyingi.

Mgomo huo ulitokana na hatua ya Shirikisho la Mpira wa Miguu uliporuhusu kuanza kwa mfumo wa kutumika kwa timu kutoka mataifa 16 kushiriki katika fainali hizo za mwaka 1966, mgomo ambao ulifungua njia ya Afrika kuongezewa idadi ya timu katika michuano hiyo.

Ni katika fainali  hizo ambapo  wapenzi wa mchezo huo walishuhudia  bao la ajabu  lililofungwa na  Mreno mwenye asili ya Afrika, (Msumbiji), Eusebio  dhidi ya Korea Kaskazini na kutoa onyo kwa mataifa ya Ulaya kuwa hata Waafrika wanaweza

 Kususia kwa Bara la Afrika ulikolea pale nchi za Ulaya zilipopewa  nafasi ya kuwa na timu 10, akiwemo na mwenyeji Uingereza, nne kutoka mataifa ya Amerika Kuisni na moja kutoka Amerika ya Kati na Carribbean.

Kutokana na mahesabu hayo  ilibaki nafasi moja iliyokuwa ikitakiwa kugombaniwa na  mabara matatu ya Afrika, Asia na Oceania hali iliyoifanyaAfrika kususia kwa nia ya kusisitiza uwepo wa usawa katika mgawanyo huo.

Hali hiyo ilimfanya Mkurugenzi wa michezo wa Ghana, wakati huo Ohene Djan, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Fifa, kupaza sauti kupiga hatua hiyo ya FIFA ya kuendekeza ubaguzi kama huo.

“Nawasilisha pingamizi langu zito kwa maamuzi ya FIFA yasiyokuwa na usawa wa mgawanyo wa nafasi katika usawa katika  mashindano  haya kwa mabara ya Afrika, Asia na Oceania, hili lisimame,” alilalamika katika ujumbe wake wa telegram alioutuma kwenda FIFA.

Malalamiko  hayo yalichagizwa na Rais wa Ghana wa wakati  huo  Kwame Nkrumah kwa kutoa wito kwa FIFA kuangalia upya uamuzi wake juu ya mgawanyo huo wa timu za kushiriki katika michuano hiyo.

Nkrumah alitaka kutumia mchezo wa  soka kwa ajili ya kuiunganisha Afrika na alimwambia mshirika wake, Djan kufanya lolote litakalofaa kuliweka soka la Afrika katika uso wa dunia na njia pekee ilikuwa ni kupata uwakilishi kombe la dunia.

 Djan na mwenzake, Tessema Yidnekatchew, raia wa Ethiopia ni miongoni mwa watu waliochangia  kwa kiasi kikubwa Bara la Afrika kuongezewa uwakilishi  katika michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Urusi.

Kutokana na msimamo huo wa mataifa ya Afrika wa kugomea michuano hiyo Afrika ilitambuliwa na sasa ina nafasi tano za ushiriki wa Kombe la Dunia inayohusisha mataifa 32 katika fainali. Kwa mara ya kwanza mashindano haya yamefanyika Afrika nchini Afrika  Kusini mwaka 2010.

Tayarin Rais wa sasa wa FIFA, Gianni Infantino anafikiria kuongeza idadi ya washiriki kutoka nchi 32 hadi kufikia 48 katika mwaka 2026, hivyo Afrika na Asia watapata nafasi nyingi zaidi.

Katika mashindano hayo Africa itapata nafasi – 9 (kutoka 5), Asia – 8 (kutoka 4 au 5), Ulaya – 16 (kutoka 13), North, Central America na Caribbean – 6 (kutoka 3 au 4), Oceania – 1 (kutoka 0 au 1) na South America – 6 (kutoka 4 au 5).