Mahakama ya Wilaya Karagwe imemtia hatiani Afisa Mifugo wa Kijiji cha Nyaishozi – Mwenge Datius Mathias.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la kupuuza wajibu wa kikazi kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kupewa adhabu ya kutofanya kosa ndani ya miezi kumi na miwili (conditional discharge) na kurejesha fedha za halmashauri shilingi 2,282,500/= . Fedha hizi hakuwa ameziweka benki baada ya kukusanya kwa njia ya POS ambapo ameamriwa ndani ya miaka mitatu awe amekwisha zilipa.
Hukumu hiyo katika shauri la jinai Namba 14808/2024 imetolewa na Mhe Flora Haule Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Karagwe June 20, 2024.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili Mwandamizi Richard Malekano huku mshtakiwa akijiwakilisha mwenyewe.