Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA, Dar es Salaam

Taasisi ya African Future Foundation (AFF) ya nchini Korea itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila) ili kuongeza ujuzi na weledi kwa watalaamu wa Hospitali hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Rais wa Taasisi hiyo, Dkt. Park Sang Eun alipomtembelea Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi ili kujadiliana juu ya mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya AFF na MNH-Mloganzila.

Prof. Janabi amesema ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili umekua wa manufaa na kwamba sasa unaenda hatua nyingine ya kutengeneza makubaliano mapya katika maeneo kadhaa yakiwemo ya mafunzo na utoaji huduma hususani kujengeana uwezo kwa watalaamu ambapo AFF inafanya kazi kwa nchi za Afrika.