Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia, Dar es salaam
SIKU chache baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji nchini , Uongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo umeibuka kupinga matokeo hayo na kuwataka viongozi wao katika ngazi hizo wasitoe ushirikiano kwa viongozi ambao wamechaguliwa.
Pia amesema kwa sasa ACT Wazalendo wanajipanga kuzungumza na asasi za kiraia na vyama vya siasa makini ili kujadiliana hatua za pamoja za kuchukua ili kuhakikisha mchakato huo wa uchaguzi unarudiwa kutokana na madai kwamba haukuwa wa haki.
Hayo yamebainishwa Novemba 29,2024 na kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kudai kwamba katika maeneo mengi vitendo vingi visivyokuwa vya kiungwana vilitendeka na vinegar wa ACT walipojaribu kuzuia walishughulikiwa vilivyo.
“Hivyo kutokana na changamoto ambazo zimejitokeza ACT tunatoa msimamo wa awali kwamba hatukubaliani na matokeo ambayo yametangazwa kutokana na machakato mzima kuvurugwa, kulingana na hayo tunataka ubatilishwe na uchaguzi mpya ufanyike.
“Pia tunataka baadhi ya maeneo yafanyiwe kazi kwa pamoja na vyma na asasi makini ni mabadiliko ya katiba ili kupata Katiba Mpya, Sheria za uchaguzi na uundwaji wa tume huru ya uchaguzi pamoja na sekretarieti huru ya tume ya uichaguzi wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi, makarani yote hayo yakamilikekabla ya uchuguzi mkuu ujao,” amesema.
Ameongeza kuwa kwa sasa ACT wanaendelea kukusanya taarifa ya matukio yote yaliyofanyika na baada ya hapo watatoa taarifa ya kamili ya chama kuhusu uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji ambao umefanyika.