Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam

Chama cha ACT Wazalendo kimeishauri Serikali kushughulikia tatizo la upatikanaji wa mawasiliano ya simu, intaneti na matangazo ya Televisheni na Redio limekuwa kwani limekuwa likirudisha maendeleo ya maeneo ya vijijini na baadhi ya miji.

Ushauri huo umetolewa leo Mei 19 ,2024 na Rahma Mwita Waziri Kivuli wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi Waziri kivuli wakati akichambua Bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mwaka wa Fedha 2024/2025] iliyowasilishwa Mei 16, 2024 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Moses Nnauye )amesema taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 na Mpango wa Makadrio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka wa fedha 2024/2025.

Waziri kivuli ACT Rahma amesema kwa mujibu wa taarifa za uchambuzi wa wizara ya mwaka 2023 ambao umetumika katika Bajeti hii ya 2024/2025 ni kuwa asilimia 69 ya ardhi ya Tanzania (Geographical Coverage) imefikiwa na huduma ya mwasiliano ya simu za kiganjani. Uchambuzi wa wizara wa mwaka 2022 nao ilikua asilimia 69, hii inamaa na kuwa kuna ongezeko la asilimia sifuri (0%).

“Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya huduma ya intaneti yanakua siku hadi siku hadi kufikia Mwezi Aprili 2023 watumiaji wa huduma za intaneti nchini ni Milioni 33.1 ongezeko la asilimia 10.7 kutoka mwaka 2022.


Katika mazingira ambayo sekta hii inakua kwa kasi hii bila kuratibu na kusimamia vizuri viwango vya huduma na gharama zake ni kuruhusu wananchi wako kunyonywa na kupitia mateso makubwa bila ungalizi na kuwaacha bila ulinzi ” amesema Rahma.

Hata hivyo ACT Wazalendo imeishauri Serikali kufanya marekebisho ya kanuni zinazosimamia vifurushi vya dakika za kupiga, mitandao (intaneti) na meseji ili kushusha gharama pia kuongeza ushirikishwaji wa wananchi ili kuwezesha kudhibiti, uholela wa Kampuni hizo kupandisha gharama vile watakavyo.


na Serikali ianzishe mchakato wa kutengeneza upya Sera ya taifa ya mawasiliano kwa kuwashirikisha kikamilifu watoa huduma, watumia huduma, wataalamu wa masuala ya kimtandao na wadau wengine.

Sambamba na hayo amefafanua kuwa Mawasiliano ya simu na intaneti (mtandao) takwimu zinaonesha wananchi asilimia 31 hawapati huduma ya mtandao wa simu pia, kuna zaidi ya vijiji 2,212 vyenye changamoto ya mawasiliano nchini mpaka kufukia April 2024 ni vijiji 616 tu ndio vilifikiwa na huduma ya mawasiliano kwa kujegewa minara , na kwamba Katika mwaka wa fedha 2023/24 ni Minara 124 tu ndio dishwasher katika minara 758 inayojengwa kwenye kata 73 hali hii inaumiza kuona bado kuna viijiji nchini havina kabisa mawasiliano ya simu katika karne 21.

Pia kwa upande wa upatikanaji huduma ya intaneti ndio imekuwa changamoto kubwa zaidi vijijini. Ikiwa kuna vijiji havijafikiwa na huduma ya kawaida ya simu (Kupiga, kupokea na meseji) basi ni wazi havina intaneti. Vile vile hata vijiji ambavyo vimefikiwa na huduma ya intaneti kasi yake ni ndogo vipo kwenye kizazi cha pili au tatu ( 2G au
3G).

Waziri Kivuli ACT amebainisha kuwa yapo maeneo mengi hapa nchini hayapati kabisa huduma za matangazo ya Redio ya TBC au Televisheni na kuna wilaya 9 hazina usikivu wa uhakika wa redio kama vile ikiwemo Kilosa, Longido, simanjiro, wanging`ombe, Mbogwe, kishapu, madaba, Mpimbwe, Itigi huku usikivu katika wilaya 29 ni wa kusuasua.hivyo tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa maeneo ya mipakani mara nyingi wanasikiliza Redio za nchi jirani inasikitisha katika miaka sitini na tatu ya uhuru wa nchi yetu, wapo wananchi ambao wameachwa nyuma kiasi cha kutokuwa na uwezo wa kupata habari kwa simu au redio ama televisheni.

“Niseme kuwa changamoto hizi, humalizwa kwa serikali kuamua kuwekeza kwa kutenga fungu la fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mawasiliano vijijini ni wa uhakika tunatoa rai kwa Serikali katika mwaka huu na miaka ijayo ihakikishe Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) unatengewa fedha za kutosha ili kuimarisha mtandao wa mawasiliano nchini” amesema Waziri Kivuli Rahma

Aidha Act Wazalendo sehemu kubwa ya maisha ya Watanzania hasa wa mijini wamekua wakiitumia katika kufanya, kufanya biashara mtandaoni, kuagiza na mizigo kutoka nje ya nchi, kufanya miamala, kupata huduma mbalimbali zikiwemo za Serikali kupitia mfumo wa huduma za Serikali kidigitali.