Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam

CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema wagombea wa vyama vya upinzani katika maeneo mengi nchini wamekuwa wakinyimwa fomu za kuwania uongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa mwishoni jana na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara Isihaka Mchinjita akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Amebainisha wakati mwingine watendaji wa vijiji wa Mitaa wamechukua hatua ya kuwakimbia wagombea ili wasichukue au wasirudishe fomu hizo.

Akielezea dosari katika uchukuaji fomu amesema “Maeneo mengi wanachama wa ACT wamejitokeza kuchukua fomu lakini wanapewa nakala moja na hivyo wanatakiwa wakatoe ‘photocopy’.

Mchinjita kudai kuwa wasimamia wamefikia hatua ya kukimbia ofisi na hawapatikani na maeneo mengine wasimamizi hudai kuwa wameshatoa fomu Kwa wagombea wa ACT huku wakijua sio kweli.

Kadhalika amedai kuwa wagombea wamekuwa wakitishiwa kwamba wasichukue fomu wala kugombea, lakini pia Kwa waliogombea wakitakiwa wajitoe.

Kwamba wagombea pia wamekuwa wakidaiwa vitambulisho vya uraia huku wakitambua kua sio wote wenye vitambulsho hivyo wamuomba Waziri wa Tamisemi mwenye dhamana hiyo kutoa tamko katika maeneo yote kulikooneka dosari.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuitaka Serikali Kwa muda uliobaki kuhakikisha wagombea wote wanapatiwa fomu na kijirejesha bila vikwazo.