Wakati presha ya usajili wa wachezaji wapya kwa klabu za hapa Tanzania ukiendelea kushika kasi, Mwenyekiti wa Kamati Maluum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abass Tarimba, amesema jukumu kubwa la Kamati hiyo ni kushauri.
Tarimba ameeleza kazi hiyo wanaifanya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendani ndani ya klabu pamoja na ile ya usajili ili kuhakikisha mipango yote inaenda sawa.
Mwenyekiti huyo ameeleza kwa sasa watakuwa wanafukuza mwizi kimyakimya na hawatoweza wazi kiasi cha miamala yao yote itakayokuwa inafanyika.
Tarimba amesema wataenda kimyakimya kutokna na matamko ya uongozi wa klabu hiyo hivi karibuni wamekuwa wakikataa kutaja wachezaji walio kwenye mipango yao ya kuwasajili sababu wamekuwa wakisajiliwa na timu zingine.
“Kamati yetu sisi ni ya ushauri, ni kamati ambayo imepewa mamlaka hayo kupitia Mkutano Mkuu uliofanyika, lengo letu itakuwa ni kumfukuza mwizi kimyakimya, hatutakuwa tunatangaza wazi miamala itakayokuwa inafanyika” alisema.
Kwa mujibu wa Tarimba ameahidi kamati yao kutekeleza kazi yao hiyo maalum pamoja na kuwa sehemu ya ushauri kwa viongozi wa Yanga kupitia Kamati ya Utendaji na Usajili.