Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupiga picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.
Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni nchini Urusi.
Ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.
Mwaka 2010, lilipokelewa na rais wa wakati huo Mwai Kibaki ambaye alistaafu mwaka 2013.
Kenya ni ya 21 mwaka huu kuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka huu kati ya mataifa 51 yanayotarajiwa kulipokea kabla ya Juni.
Kombe hilo ambalo lina uzani wa kilo 6.1 limeelekea Maputo, Msumbiji.
Wakati wa kuwasili kwa kombe hilo Jumanne, wacheza ngoma waliovalia mavazi ya kitamaduni ya jamii ya Wamaasai walikuwepo kuwatumbuiza wageni.