Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetoa Jumanne ripoti yake ya kila mwaka na kukosoa vikali hatua za rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ametimiza siku 100 akiwa madarakani.

Amnesty imesema hatua za Trump zinalenga kurejesha nyuma mafanikio yaliyopatikana katika vita dhidi ya umaskini duniani, kupambana na ubaguzi wa rangi na vipaumbele muhimu vya haki za binadamu.

Tangu alipoapishwa kuongoza muhula wa pili mnamo Januari 20, Trumpamechukua hatua kadhaa ambazo zimeutikisa ulimwengu kiuchumi, kijamii na kiusalama.

Baadhi, ni hatua za ushuru, kusitisha misaada ya kimataifa, sintofahamu na washirika wake wa NATO pamoja na vitisho vya kunyakuwa maeneo kama Gaza, Greenland, Mfereji wa Panama na kutaka kuifanya Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.