Waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi Sergey Lavrov amesema kuwa Urusi iko tayari kusitisha mapigano bila masharti, lakini “tunataka hakikisho kwamba usitishaji mapigano hautatumika tena kuimarisha jeshi la Ukraine na kwamba usambazaji wa silaha lazima ukome.”
Akizungumza na mwandishi wa habari aliyehoji kwamba Kyiv ilikubali pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano kabisa Machi 11, lakini Moscow iliweka masharti.
Bwana lavrov alijibu: “Hapana, haya sio masharti,”. “Haya ni masomo ambayo tumejifunza angalau mara tatu, wakati mikataba inayofanana na tunayojadili sasa ilihitimishwa”
(Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi alikuwa akimaanisha mikataba ya kusitisha mapigano iliyohitimishwa huko Minsk, ambayo Kyiv na Moscow wanashutumu kila mmoja kwa kukiuka).
Lavrov amesema kwamba kwa usitishaji mpya wa mapigano nchi za Magharibi lazima ziache kuipatia Ukraine silaha.
Kyiv na washirika wake wa Ulaya hapo awali waliita hali hii kuwa haikubaliki, kwani Ukraine ingekuwa bila ulinzi mbele ya mchokozi.
“Utawala wa Ukraine unaungwa mkono na miji mikuu ya Ulaya na utawala wa Biden Ikiwa unataka kuanzisha usitishaji vita na kuendelea tu kusambaza silaha kwa Ukraine, lengo lako ni nini?”
Kulingana na Lavrov, Ulaya “ilisema moja kwa moja kwamba inaweza tu kuunga mkono makubaliano ambayo hatimaye yataifanya Ukraine kuwa na nguvu zaidi, ambayo itaifanya Ukraine kuwa mshindi.”
“Kwa hivyo ikiwa hilo ndilo dhumuni la usitishaji vita huu, sidhani kama hivyo ndivyo Rais Trump anataka.
Hivyo ndivyo Wazungu, pamoja na Zelensky, wanataka kufanya kuhusu mpango wa Rais Trump.”
