Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inalojukumu la kuhakikisha uchaguzi Mkuu unafanyika kwa amani na haki.
“Wito wangu kwa kanisa ni kuendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani,” amesema na kuongeza kuwa atamtaatifu Mhe. Rais kuhusu ahadi ya maaskofu kuliombea taifa hili kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
Dkt. Biteko amesema hayo Aprili 27, 2025 Iringa Mjini alipomwakilisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni maalum katika sherehe ya kusimikwa na kuwekwa wakfu kwa Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali.

