Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwa sasa rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine anaonekana kuwa mtulivu na mwenye nia ya kutaka kufikia makubaliano ya amani.

Aidha Trump ameusifu mkutano wao siku ya Jumamosi mjini Vatican, huku akimtaka pia rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha mashambulizi nchini Ukraine na kukaa kwenye meza ya majadiliano ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kauli za Trump zimetolewa wakati Moscow na Kiev zikiendelea kushambuliana vikali kwa makombora na droni, huku Korea Kaskazini ikithibitisha kuwa imewatuma wanajeshi wake nchini Urusi kusaidia katika vita hivyo hasa katika ukombozi wa eneo la mpakani la Kursk.