Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Musoma
WAVUVI wawili kati ya wanne waliozama ziwa Victoria usiku wa Aprili 21,2025 bado hawajapàtikana licha ya juhudi za kuwatafuta.
Akizungumza kwa njia ya simu na Jamhuri Media mmiliki wa mtumbwi waliozama nao wavuvi hao waliokuwa wakimfanyia kazi Silas Adam Maingu ameiomba Serikali kusaidia kuwatafuta wavuvi hao kwani wao wamefanya jitihada lakini bado hawajafanikiwa
“Tumefanya kila iwezekanavyo na watu waliokuwa wakinifanyia kazi za uvuvi kuwatafuta kwa huku tushirikiana na familia zao pamoja na jamii iliyotuzunguka bila mafanikio”amesema Maingu.
Silas amesema wavuvi hao walizama siku ya Aprili 21, majira ya usiku walipokuwa wakiendelea na shughuli zao za uvuvi kwenye Kisiwa cha Rukuba.
Amesema kati ya wavuvi hao mmoja aliyepatikana ni Makebe Nyarubamba alikutwa akiwa amekufa maji na ambao mpaka sasa hawajulikani walipo ni hadi sasa Revocatus Mtega Pulizo na Fedrick Matiku na Cleophace Bahati Mganga
Silas anayejishughulisha na shughuli hizo za uvuvi katika Kisiwa cha Rukuba amewaomba wanaojishughulisha na uvuvi na kutumia ziwa Victoria kutoa taarifa watakapoona miili ya wavuvi hao kwa kuwa wanaweza kuonekana tofauti na walipozamia.
” Tunaendelea na juhudi za kuwatafuta ndugu zetu waliozama ziwa Victoria usiku wa aprili 21 Kisiwa cha Rukubwa wakiwa kwenye majukumu ya kazi.
” Tunaiomba serikali pia itisaidie lakini pia wavuvi ziwa watakapofanikiwa kulma miili yao maeneo yoyote watufahamishe,amesema Silas.
Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Mara Mrakibu Augustine Magere amesema wamefanikiwa kumpata mtu mmoja siku ya jana na jitihada za kuwatafuta wengine wawili bado zinaendelea.
Amesema kutokana na jografia na upepo juhudi zinaendelea kwa kushirikiana na watumiaji wengine wa ziwa Victoria wakiwemo wavuvi.
