Upinzani nchini Uturuki, umewataka wafuasi wake kukusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Ankara leo Jumatano, kupinga marufuku iliyotangazwa rasmi dhidi ya mikusanyiko.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHP, Ozgur Ozel, amesema atahutubia nje ya bunge wakati nchi hiyo ikiadhimisha leo siku ya uhuru wa taifa.

Ozel amewaambia wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi leo alasiri akisisitiza kwamba raia ndiyo wenye mamlaka ya taifa hilo.

Meya aliyekamatwa mwezi mmoja uliopita, kwa tuhuma za rushwa, Ekrem Imamoglu, ambaye ni mgombea urais wa chama cha CHP mwaka 2028, pia ametowa mwito akiwa gerezani wa kutaka waturuki washiriki maandamano hayo.