Chama cha ACT- Wazalendo kimepokea kwa huzuni na masikitiko kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis kilichotokea leo.
Taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu imemuelezea Papa Francis kuwa alikuwa kiongozi mnyenyekevu aliyehubiri haki na kutafuta amani duniani hasa Afrika.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Papa alikuwa na kiongozi mwenye ubinadamu kwa kila mtu bila kujali tofauti za kiimani.
Papa Francis alikuwa kiongozi wa kiroho mwenye utu, asiyejikweza na aliyeguswa na madha na umasikini wa watu na alipenda dunia kuchukua jitihada za makusudi kuondoa umasikini miongoni mwa jamii ya binadamu,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
ACT imetoa pole kwa waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania na kote duniani, hivyo chama hicho kinaungana na walioguswa na msiba huo na kuwaombea heri.
