Papa Francis amejitokeza katika Uwanja wa St Peter mjini Vatican kuwatakia “Pasaka Njema” maelfu ya waumini.
Papa, 88, alitoka kwa kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye roshani ya St Peter Basilica na kushangilia umati wa watu, akisema: “Ndugu na dada, Heri ya Pasaka.”
Hotuba yake ya kitamaduni ya Pasaka ilitolewa na mshiriki wa dini.
Baada ya baraka, Papa alizungushwa uwanjani akipita katikati ya umati, msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki.
Kuonekana kwake Jumapili ya Pasaka kulikuwa kumetarajiwa sana.
Mwezi uliopita, aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya wiki tano za matibabu kwa maambukizi ambayo yalisababisha matatizo ya kupumua mara mbili.
