Watu wenye silaha wamefanya mauaji ya takriban watu 56 mapema wiki hii katika jimbo la Benue katikati mwa Nigeria, ofisi ya gavana ilisema Jumamosi, ikirekebisha kwa kasi idadi iliyotolewa awali ya watu 17.
Viatu vilizosalia vya wanafunzi wa Shule ya Upili ya Bethel Baptist vinaonekana ndani ya eneo la shule huku wazazi wa wanafunzi waliotekwa nyara wakisubiri kurejeshwa kwa watoto wao ambao walitekwa nyara na watu wenye silaha katika Eneo la Serikali ya Mtaa ya Chikun katika jimbo la Kaduna, kaskazini-magharibi mwa Nigeria Julai 14, 2021.
Mapigano kati ya wafugaji wa kuhamahama na wakulima kuhusu matumizi ya ardhi ni ya kawaida katikati mwa Nigeria.
Awali gavana wa eneo hilo Hyacinth Alia alionesha kuwanyooshea kidole jamii ya wafugaji kuhusika na vurugu za maeneo ya Ukum na Logo.
Kwa vile wafugaji wengi watoka katika jamii ya Kiislamu ya kabila laFulani,na wakulima wengi katika uumini wa Kikristo mashambulizi katika eneo linaloitwa Middle Belt mara nyingi huchukua mwelekeo wa kidini au kikabila.
