Rais Volodymyr Zelenskiy katika Jumapili hii ya Pasaka ametaka Waukraine kutokata tamaa ya kupatikana kwa amani,akisema watarejea katika nchi yao na wavumulie kuishinda nyakati ngumu ya vita iliyodumu kwa siku 1,152.

Akiwa amevaa shati la kijivu lenye nakshi ya Kiukraine, mbele ya kanisa kubwa la mjini Kyiv, la Mtakatifu Sophia, Zelensky kwa kupitia mitandao ya kijamii, amesema Ukraine kamwe haitapoteza imani.

Awali Jumamosi Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza siku moja kusitisha mapigano katika ardhi ya Ukraine kwa ajili ya Pasaka – ambayo kwa mwaka huu imeangukia siku moja kwa madhehebu ya Orthodox na Makanisa ya Magharibi.

Lakini mapema Asubuhi ya leo Rais Zelenskiyalisema jeshi la Urusi linaigiza kusitisha mapigano huku likiendelea na mashambulizi yake usiku kucha kuisababishia athari katika maeneo ya vita ya Ukraiine.