Na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ameipongeza Mamlaka ya Bandari kwa kazi nzuri ya kuboresha huduma na kuongeza ufanisi, hali inayoifanya Tanzania kuvutia zaidi kibiashara.
Chalamila amesema kuwa bandari hiyo imekuwa kivutio kikubwa kwa mataifa jirani na mbali, kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa, ikiwa ni pamoja na ongezeko la malori ya mizigo na wageni wanaochukua bidhaa zao kupitia bandari ya Dar es Salaam.
“Wakati vyama vingine vikikejeli uwekezaji katika bandari, sisi tunaona matokeo na maendeleo makubwa yanayoendelea kufanyika katika bandari yetu,”anasema Chalamila.
Chalamila ameeleza kuwa wageni wanakuja, mizigo inapita, uchumi unakua haya ni mafanikio makubwa sana,” alisema Chalamila.
Aidha amesisitiza kuwa amesisitiza kuwa bandari hiyo ni lango kuu la biashara Afrika Mashariki na inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania.

.