Na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert chalamila, amesema kuwa katika kutatua changamoto sugu ya mafuriko eneo la Jangwani ujenzi wa daraja jipya utaanza rasmi mwaka huu.

Chalamila amesema hayo leo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam “mkandarasi tayari ameanza maandalizi ya kuweka vifaa katika eneo la mradi, na Waziri wa TAMISEMI amethibitisha kuwa ujenzi utaanza karibuni”amesema Chalamila.

Aidha ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa daraja hilo, wakazi wa Jangwani na maeneo jirani hawatateseka tena kila mvua zinaponyesha.

“Hili daraja litakuwa suluhisho la mafuriko, lakini pia litakuwa sehemu ya kupendezesha jiji letu na kurahisisha usafirishaji,” alisema Chalamila.


Aidha, alieleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea hususa ni madaraja yaliyoharibiwa na mvua.