Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Watanzania kwa kasi kubwa wanaanza kukumbatia utamaduni wa kusafiri ndani ya nchi, ingawa bado haujafikia kiwango au marudio ya mara kwa mara yanayoonekana katika mataifa ya Magharibi.

Kwa mujibu wa Chama cha Kuendeleza Utalii Afrika (APTA), asilimia 60 ya shughuli za utalii mwaka 2024 zilihusisha watalii wa ndani. Ongezeko hili kubwa linaashiria mwelekeo mpya na unaokua wa Watanzania kuchagua kutumia mapumziko yao hapa nchini.

Kwa kampuni ya usafiri wa mtandaoni ya Bolt Tanzania, hali hii ina maana ya kutarajia ongezeko la usafiri wakati wa sikukuu kama Pasaka, na kutoa fursa kwa wasafiri kunufaika na ofa maalum pamoja na huduma ya “Scheduled Rides” — inayowezesha upatikanaji wa usafiri kwa wakati waliopanga. Huduma hii inalenga kusaidia watumiaji kufika kwa urahisi maeneo kama migahawa, hoteli, bustani, hifadhi za wanyama na vituo vya mapumziko.

Mwaka 2024, Tanzania ilirekodi zaidi ya watalii wa ndani milioni 3.2, na hivyo kuzidi idadi ya watalii wa kimataifa waliokadiriwa kuwa milioni 2.1. Ongezeko hilo limechangiwa na kampeni maalum kama #UtaliiTena, ambayo inawahamasisha wananchi kutembelea vivutio vya ndani, sambamba na juhudi za serikali za kuhimiza utalii wa ndani.

Mwaka huu wa 2025 pekee tumeshuhudia shughuli nyingi za mapumziko kutoka kwa wananchi, jambo linalothibitisha ukuaji wa utamaduni wa kusafiri ndani ya nchi,” alisema Dimmy Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya.

“Tulifikia kilele cha safari wakati wa Valentine mwezi Februari, safari zikazidi mara mbili katika mkoa wa Moshi wakati wa Kilimarathon, na sasa tunaona ongezeko la asilimia 12 la safari zilizopangwa kuelekea Pasaka.

Licha ya ukuaji huu wa matumaini, changamoto bado zipo. Wengi bado wanaona usafiri kama anasa, inayohitaji gharama kubwa au kuhifadhiwa kwa hafla maalum kama harusi au mikutano ya kifamilia. Sababu za kiuchumi, kama mapato ya kaya na gharama za usafiri, bado zinaathiri maamuzi ya kusafiri. Pia, kuna uhitaji wa kuongeza uhamasishaji na matangazo ya vivutio vya ndani ili kuchochea hamasa zaidi miongoni mwa wananchi.

Kwa mujibu wa Bolt Tanzania, huduma ya “Scheduled Rides” kwenye programu yao inawawezesha watumiaji kuhifadhi usafiri kati ya dakika 30 hadi siku 90 kabla, hivyo kusaidia kujenga utamaduni wa kupanga mapema na kuhakikisha upatikanaji wa dereva kwa wakati unaotakiwa.