MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Muadhama Kadinali Protase Rugambwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Wasira amekutana na Protase Kardinali Rugambwa. leo Aprili 16, 2025 katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani Tabora.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na ustawi wa Tanzania.

Aidha, baada ya mazungumzo yao Wasira ametembelea Shule ya Sekondari ya St Marrys (Mihayo) iliyopo mjini Tabora.

Shule ya Sekondari ya St. Mary’s imebeba historia kubwa kwani ndiyo Shule ya kwanza ambayo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifundisha kwa miaka mitatu.