Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi ya Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 CAG imebainisha kuwa mashirika 19 ya umma ya kibiashara yameendelea kupata hasara, huku mashirika 12 yakipata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG mashirika 10 ya umma yaliyoingiza hasara kubwa zaidi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni pamoja; –

1 Shirika la Reli Tanzania (TRC) Hasara ya (Sh bilioni 224.59)
2 Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) (Sh bilioni 91.80)
3 Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (Sh bilioni 27.78)
4 Shirika la Posta Tanzania (Sh bilioni 23.64)
5 Kampuni ya Mkulazi Holding Ltd Sh bilioni 19.04
6 Kampuni ya Ngozi Kilimanjaro Sh bilioni 5.05
7 Kiwanda cha Bidhaa za Kibiolojia Sh bilioni 4.26
8 Kampuni ya Magazeti ya Serikali Sh bilioni 3.51
9 Kampuni ya Sisalana Tanzania Sh bilioni 2.44
10 Kiwanda cha Madawa Keko Sh bilioni 1.84