Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametembelea na kufanya mazungumzo na timu ya uongozi wa Bandari ya Kimataifa ya Antwerp iliyopo nchini Ubelgiji ukiongozwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bandari hiyo Bw. Stefan Cassimon. 

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na Bandari ya Kimataifa ya Antwerp, hususan katika maeneo ya usimamizi wa bandari, fursa za uwekezaji, na programu za kujenga uwezo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bandari ya Kimataifa ya Antwerp Bw. Stefan Cassimon alipotembelea bandari hiyo Aprili 16, 2025. 

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Kombo ameeleza kuhusu umuhimu wa Mamlaka hizo mbili za Bandari kushirikiana, akitaja kuwa pamoja na masuala mengine itasaidia kuongeza wigo wa soko na ufanisi kwa manufaa ya pande zote mbili. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bandari hiyo Bw. Stefan Cassimon ameeleza kuhusu utayari wa Bandari hiyo wa kushirikiana na Tanzani katika masuala ya uendeshaji na usumamizi wa bandari, akisisitiza kuwa hatua hiyo itakuwa ni kichocheo cha maendeleo ya uendeshaji wa bandari kwa mfumo kisasa na tija zaidi. 

Waziri Kombo amehitimisha ziara yake ya kikazi katika Umoja wa Ulaya (EU) ambayo aliianza Aprili 14, 2025. 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na uongozi wa Bandari ya Kimataifa ya Antwerp Aprili 16, 2025
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na ujumbe wake wakifuatilia wasilisho kuhusu historia na uendeshaji wa Bandari ya Kimataifa ya Antwerp kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Bandari hiyo Bw. Stefan Cassimon.