Na Christopher Iilai, JamhuriMedia, Lindi

Serikali imesitisha uazishaji wa vyama vya ushirika kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na badala yake vyama vilivyopo vijikite katika kujihimarisha kiuchumi ile viweze kuiiendesha.

Hayo yamesemwa na Mrajis wa vyama vya ushirika nchini,Dr Benson Ndiege kwenye mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI nilichofanyika wilayani Liwale ambapo alibainisha kuwa kumekuwa na kasi ya kuomba kuanzisha vyama vipya ambavyo vinatokana na kugawanyika kutoka kwenye vyama vya ushirika vilivyopo.

Dk Ndiege amesema kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara vyama vilivyopo vinatosheleza na kuwa lengo la ushirika ni kuwa na ushirika wenye nguvu sokoni.

Amebainisha kuwa kuna timu ambayo itaanza kufanya tathmini ya uwepo wa vyama vya ushirika ili kubaini kama kuna vyama ambavyo haviwezi kujiendesha ili viunganishwe na kama kuna chama ambacho kikubwa basi itatolewa kibali cha kuanziasha chama kingine.

“Furaha yangu ni kuona ushirika wenye nguvu na sio kuwagawa na nitakuwa mtu wa mwisho kufikiria RUNALI inagawanyika”alisema Dr Ndiege.

Aidha msajir huyo wa ushirika amewataka viongozi wa ushirika nchini kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria, miongozo, masharti na maelekezo yanayosimamia ushirika.


Wakati huo huo mrajis huyo amezindua mradi wa usafirishaji ambapo RUNALI imenunua magari manane yenye thamani ya zaidi ya sh billion 1 na mia tatu ambayo yatatumika kusafirishia mazao ya wakulima.

Dr Ndiege ameipongeza bodi ya chama kikuu hicho cha RUNALI kwa kuanzisha mradi huo ambao unaendana na kaulimbiu ya Ushirika ni biashara.