Wachezaji wa Morocco

Wachezaji wa Morocco washerehekea baada ya kuifunga Nigeria na kulinyanyua taji la CHAN 2018 nyumbani

Michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani ( CHAN) imehitimishwa Jumapili kwa ushindi wa wenyeji Morocco waliofanikiwa kulinyanyua taji la michuano hiyo kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nigeria.

Mchezaji wa Morocco Zakaria Hadraf alifanikiwa kupachika wavuni bao la kwanza muda mfupi kabla ya kipindi cha mapumziko huku mchezaji wa Nigeria Peter Eneji Moses akitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano muda mfupi baad ya bao hilo.

Walid El Karti na Hadraf – katika bao lake la pili – waliipatia Morocco uongozi katika mechi hiyo kufikia dakika sitini.

Kampeni hiyo ilikamilishwa kwa bao la Ayoub El Kaabi, aliyegonga chuma mara mbili , na kufanikiwa kulifunga bao lake la tisa katika mashindano hayo ya wachezaji wa nyumbani wa timu za Afrika.

Nafasi ya kwanza ya Morocco ilikuja kunako dakika tatu za mechi wakati Walid El Karti aliposukuma tobwe katika eneo la karibuna lango kuu.

Wenyeji hao walidhani wameshafunga bao lao la kwanza katika dakika ya nne alipoisakata ngozi , kwa bahati mbaya naibu refa akanyanyua bendera akidai kiki hiyo ilisukumwa vibaya kabla ya kumfikia mshambuliaji huyo.

El Kaabi akasukuma hedi na kipa wa Nigeria Oladele Ajiboye ilibidi aokoe matobwe mawili kabla ya shinikizo la Morocco kujipa.

Kwa ukubwa Nigeria ilitegemea pasi ndefu kwa mashambulio yao na Anas Zniti wa Morocco hakuwana kibarua kikubwa kuokoa kabla ya muda wamapumziko.

Dakika mbili baada ya kipindi cha mpumziko Peter Eneji Moses alitimuliwa uwanjani baada ya kupewa kadi ya pili ya njano kwa mchezo m’baya dhidi ya Mohammed Nahiri.

Morocco ikaongeza bao la pili kunako dakika sitina wakati kiki ya El Kaabi ilipogonga chuma na kurudi nyuma kumwezesha El Haddad kusukuma kwa mara ya pili tobwe ambalo lilimfanya Ajboye asue sue na kumpa nafasi El Karti kusukuma kwa urahisi hedi ya nguvu ndani ya wavu.

Dakika tatu baadaye Hadraf alilifunga lake la pili baada ya krosi ya El Haddad kumuangukia .

Ayoub El Kaabi

Ayoub El Kaabi aliifunga Nigeria bao na kumaliza mashindano hayo kama mfungaji bora akiwa ameyafunga tisa kwa jumla

El Kaabi hatimaye alifanikiwa kulisukuma lake kunako dakikda 73 wakati mpira ulipomuangukia mguuni na kumfanya amalize mashindano hayo kama mfungaji bora akiwa amefanikiwa kuyafunga tisa kwa jumla.

Kwa kweli timu ya watu 10 ya Nigeria ilishindwa kuitishia Morocco kabisaa katika nusu ya pili.

Magoli ya El Kaabi huedna yamechangia kummulika mbele ya macho ya koca wa timu ya taifa ya Morocco Herve Renard aliyekuwa anatizama michuano huyo pembeni akitazamia kukamilisha kikosi chake tayari kwa michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi.

Siku ya jumamosi Sudani ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Libya penati 4-2 baada ya sare ya bao 1-1.

Katika hatua ya penalti , Sudan ilifanikiwa kufunga penati na kuambulia medali ya shaba katika fainali za CHAN baada ya kuibuka tena nafasi ya tatu walipokuwa waandaaji wa mashindano hayo mwaka 2011, huku Libya wakiibuka mabingwa miaka mitatu baada ya hapo.

Mataifa 16 yalishiriki michuano hiyo ambayo yalipangwa katika makundi manne, ambayo ni Kundi A-wenyeji morocco, Mauritania, Guinea na Sudani, Kundi B-Namibia , Uganda, Zambia na Ivori Coast, Kundi C-Libya Nigeria, Rwanda na Equtorial Guinea.

Kundi D -Lilikuwa na Timu za Congo ,Angola, Cameroon pamoja na Burkina Faso.