Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Simanjiro

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Fakii Raphael Lulandala kuhakikisha anampatia orodha ya wawekezaji wote waliowekeza katika vijiji ndani ya wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kufamu kazi waliozizifanya katika maeneo hayo ili kudukuma gurudumu la Maendeleo ya Jamii husika.

Hayo amebainisha jana wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sukro Kata ya Komolo Wilayani Simanjiro Mkoani humo, mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Kiria Laizer, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Baraka Kanunga Laizer, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Gracian Max Makota, ambapo alisema wawekezaji wataingia kimya kimya atawatafsiri vingine.

Sendiga amesema wilaya ya Simanjiro ndio wilaya inayoongoza kuwa na wawekezaji wengi kuliko wilaya zote za Mkoa wa Manyara, kuhusu akihoji licha ya uwepo wa wawekezaji wengi lakini bado changamoto nyingi zimeendelea kuwaelezea wananchi.

” Wilaya ya Simanjiro Ina wawekezaji wengi mno kuliko wilaya zingine za Mkoa huu lakini hawaonekani na hawsjulikani walipo , kuonekana kwao hadi watakapokua wamegombana ndio utasikia kumbe Kijiji hiki kulikua na wawekezaji kadhaa, wakishakutana na Serikali za vijiji baadhi ya Viongozi ambao sio waaminifu wanapatana nao hutowajua Wala kuwasikii , mtawajua siku kukinuka huko wakishaanza kugombana hivi hivi huwezi kuwafikia anakuja kimya kimya kamya kama kibaka” amesema Sendiga

Aidha amesema kufuatia hilo amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Fakii Raphael Lulandala kuhakikisha Mwekezaji yeyote anaye ingia atatakiwa kujitambulisha kwenye Serikali ya wilaya, na Serikali hiyo ndio itakayomtambulisha yeye kwingine wanakotqkiwa kutambulishwa.

” Lengo ni kujua anayewekeza katika Kijiji hiki ama kile ni nani, je wananchi wanamtambua, anaisaidiaje jamii inayomzunguka pale, , tuone moja ya uwekezaji wake ni halali lakini pili uwekezaji wako unatoka Kwa jamii husika, sisi tumepata bahati tangu kupata ardhi ambayo imebeba Mali nyingi chini lakini wanaoweza kunufaika wao pasipo wahusika nao kunufaika ” amesema Mkuu huyo.

Mkuu huyo amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya kumpatia orodha ya wawekezaji wote walioko kwenye kila Kijiji kuwasilisha orodha hiyo katika Kijiji chake, ambo jumla ya vijiji 56 vitawasilisha taarifa hiyo, na tumuhakiki tujue .

” Lakini pia tujue watu wa Kijiji hiko wananufaikaje na uwepo wa Mwekezaji huyo, wawekezaji wanafanya kazi zisizo na faida Kwa jamii , unakuta wananchi wana mwekezaji lakini jamii husika haina maji Wala hawasaidii kabisa sasa uwepo wake una faida gani kwa jamii , Mwekezaji lazima aache faida” aliongeza Mkuu huyo.

” Lakini pia unakuja katika Kijiji husika Kuna vijana wasomi wapo lakini utashangaa hata kazi tu ya kupiga cheap hapatiwi, vijana wapo tu Vijijini huku nao pia akina mama hawapati hata tenda ya kupika chakula kwenye ule Mradi, wataona ni bora watoe mbali chakula kuliko kuwapatia tena akina mama hao, Sasa ndio nini , lazima waliopo katika eneo la uwekezaji wawe wanufaika wa kwanza wa Mali yao, Kwa hiyo hilo tutalisimamia” amesema Mkuu Sendiga.

Hata hivyo amesema ifike mahali wawekezaji wajambue wajibu wao kwa wananchi, hata Barbara ikibomoka anasubiriwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan apeleke Fedha ya kuchonga barabara wakati wao maroli yao yanapita muda wote huku wanashindwa kweli kuchonga barabara, jambo ambalo amesema itakua ngumu kidogo kuendelea na Mwekezaji asiye na faida kwa sasa.