Idadi ya watu wanaojulikana kunyongwa mwaka jana ilikuwa kubwa zaidi katika takriban muongo mmoja, huku Iran, Iraq na Saudi Arabia zikiongoza kwenye orodha ya nchi zilizotekeleza hukumu hiyo.
Ripoti ya kila mwaka kuhusu ya hukumu za kifo ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International imesema jumla ya watu 1,518 walinyongwa duniani kote katika mwaka 2024. Hiyo ni idadi kubwa zaidi tangu mwaka wa 2015 ambapo watu 1,634 waliuawa. Takwimu hizo zinaonesha ongezeko la asilimia 32 la idadi inayojulikana ya watu walionyongwa ikilinganishwa na mwaka wa 2023.
Katibu Mkuu wa Amnesty Agnes Callamard amesema “adhabu ya kifo ni uhalifu wa kuchukiza usio na nafasi katika ulimwengu wa leo. Amnesty imesema hazijumuishi maelfu ya watu wanaoaminika kunyongwa nchini China — inayoongoza duniani katika utekelezaji wa hukumu ya kifo — na pia Korea Kaskazini na Vietnam. Iran, Iraq, na Saudi Arabia kwa pamoja zilichangia asilimia ya 91 ya watu walionyongwa mwaka jana.
Iran pekee iliwanyonga watu 972, ikiwa ni 100 zaidi ya mwaka uliotangulia. Saudia, ambako kukatwa vichwa kulitumika, iliongeza mara mbili zaidi jumla ya idadi yake ya kila mwaka kutoka watu 172 hadi karibu 345. Na Iraq iliongeza karibu manne nne zaidi idadi ya watu iliyowanyonga kutoka 16 hadi karibu 63.