Na Mwamvua Mwinyi, JamhutiMedia, Mafia
Mwenge wa Uhuru umetembelea ,kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 2.8 .
Akipokea mwenge wa Uhuru Aprili 7, 2025, kwa mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo amesema kati ya miradi hiyo 11 imekaguliwa, miradi mitatu imezinduliwa, na mradi mmoja umewekewa jiwe la msingi, kwa umbali wa kilomita 64.9 .

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi, ameonyesha kuridhishwa kwake na kupongeza usimamizi na utekelezaji wa miradi wilayani Mafia.
Alisisitiza kuendeleza uzalendo kwa kufanya kazi kwa bidii na amewahimiza wananchi kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.
” Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na utekelezaji wa miradi wilayani hapa, uuendelee kutunza miradi hii maana inatekelezwa kwa fedha nyingi. “
“Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunaishi maisha bora yanayofanywa na Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Ussi.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukabidhiwa wilayani BagamoyoAprili 8, 2025





