Umoja wa Mataifa umesema kuwa mamia kwa maelfu ya watu walilazimika kukimbia majanga ya kimazingira mwaka jana, ikiashiria haja ya kuwepo mifumo ya tahadhari ya mapema kwa dunia nzima.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa mamia kwa maelfu ya watu walilazimika kukimbia majanga ya kimazingira mwaka jana, ikiashiria haja ya kuwepo mifumo ya tahadhari ya mapema kwa dunia nzima.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa na tabia nchi WMO limesema, rekodi hiyo ya idadi ya watu waliokimbia majanga hayo ya kimazingira imetokana na takwimu zilizotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Kuchunguza Watu walioachwa bila makao IDMC. Kituo hicho kimekuwa kikikusanya takwimu tangu mwaka 2008.

Nchini Msumbiji, karibu watu laki moja waliachwa bila makao kutokana na kimbunga Chido. Mataifa tajiri pia yaliathirika huku shirika la WMO likiyataja mafuriko yaliyoukumba mji wa Valencia nchini Uhispania na kusababisha vifo vya watu 224, pamoja na mioto ya nyika nchini Canada na Marekani iliyowapelekea zaidi ya watu laki tatu kuyakimbia makaazi yao.