Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Maendeleo Benki ,Profesa Ulingeta Mbamba amesema kuwa Maendeleo Bank imendelea kutekeleza kwa vitendo mabadiliko ya teknolojia katika sekta ya Fedha kwa kuanzisha huduma ya kidigitali ijulikanayao kama “Click Bank Smile.”
Profesa Mbamba amesema hayo jijini Dar es salaam Machi 18,2025 wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Internet Banking inayojulikana kama “Click Bank Smile” itakayorahisisha utoaji wa huduma za kifedha kwa wateja wa benki hiyo kwa njia ya kisasa,Salama na rafiki kwa Mazingira.
Hata hivyo amesema kuwa kuzinduliwa kwa kuduma hiyo ya internet Banking itasaidia wateja wa benki hiyo kufanya miamala kwa urahisi,pamoja na kurahisisha zoezi la kuhesabu fedha kwenye Tellers.

“Hatua hii ya kuzindua Internet Banking ni kubwa sana kwa Maendeleo Benki kwani itarahisisha wateja kufanya miamala yao kwa urahisi,lakini pia ni njia salama kulinda taarifa za mteja,naomba muendelee kuwa wabunifu ili muendelee kutoa huduma nzuri zenye ubora kwa wateja wetu”amesisitiza Prof Mbamba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Ndg. Lomnyaki Saitabau amesema kuwa bank yake itaendelea kuunga mkono Serikali katika matumizi ya teknolojia ili kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Fedha.
Sambamba na hayo amebainisha kuwa kipaumbele cha Benki hiyo kwa mwaka 2025 ,ni kuendeleza ukuaji wa biashara kwa njia ya kidijitali ,hivyo menejiment itaendelea kubuni na kutumia teknolojia za kisasa Katia utoaji wa huduma bora kwa wateja wa Maendeleo Bank ikiwemo kuhamasha fedha kutoka benki moja Hadi nyingine,kulipia huduma na bidhaa mbalimbali,kufanya malipo ya mara kwa mara naya moja kwa moja,kuomba hundi na kadi za ATM.

” Lengo letu ni kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia wananchi wengi zaidi ikiwa ni pamoja na Wafanyabishara wadogo nawakati,wakulima,wafanyakazi, wajasiliamali wa sekta zote,
“Click Bank Smile” inatoa fursa kwa Watanzania wengi kutumia huduma za kifedha kwa njia ya kidijitali,kupunguza gharama ya uendeshaji wa biashara,pamoja na kuongeza ufanisi wa miamala ya kifedha.” amesema Saitabau.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC amesema kuwa matumizi ya huduma hiyo wateja wa benki hiyo itapunguza muda wa kusubiri kwenye foleni, gharama za kusafiri kwenda benki na kuongeza usalama wa fedha zao,nakwamba hatua hiyo ni kubwa kuelekea mifumo ya kifedha inayoendana na mahitaji ya Dunia ya sasa.



