Na Mwandishi, Jeshi la Polisi, Mlandizi
Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Wilaya ya Kipolisi Mlandizi Mrandizi Msaidizi wa Polisi (ASP) Rose Mbaga amekutana na Askari wa kikosi hicho na kuwataka kutekeleza majukum yao kwa Mujibu wa sheria ili kupunguza ajali.
ASP Rose akiongea na Askari hao amewasisitiza kutoa elimu na kuchukua hatua za kisheria kwa madaereva wanao kiuka sheria na taratibu za usalama Barabarani.

Mkuu wa kikosi hicho wilaya hiyo ameongeza kuwa endapo Askari wa watatekeleza majukum yao kikamilifu kwa mujibu wa sheria ajali katika wilaya zitakuwa historia.
Pia amewata kuchua hatua kwa baadhi ya madereva wanaozidisha abiria huku akiwataka kuendelea kusimamia muda wote watumiaji wa Barabara ili kupunguza ajali.

