Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na Mjumbe wa Tume Mhe. Magdalena Rwebangira leo  wametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa uboreshaji wa jimbo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kushuhudia mwenendo wa mafunzo hayo ambayo ni maandalizi ya zoeazi la uboreshaji wa Daftari unaotaraji kuanza Machi 17 hadi 23, 2025. (Picha na INEC).