📌Afafanua kuuuza na kununua umeme ni jambo la kawaida kwa nchi

📌Asisitiza kununua umeme kwa Mikoa ya Kaskazini kunamanufaa kwa Mikoa husika

📌Asema kukamilika kwa Mradi wa TAZA kutainufaisha Tanzania na biashara ya umeme

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba ametoa Ufafanuzi zaidi kuhusu hatua ya Serikali kununua Umeme nchini Ethiopitia kupitia Nchini Kenya hadi Namanga Mkoani Arusha utaimarisha Upatikanaji wa Umeme katika Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambayo kimsingi kwa sasa inatumia umeme unaozalishwa katika Mikoa ya Kusini.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo tarehe 10, Machi 2025 Jijini Dar es Salaam Mha. Mramba amesema ununuzi wa Umeme kutoka nchi Jirani haimaanishi kuwa nchi iko katika changamoto ya upungufu wa umeme kwa kuwa mpaka sasa Tanzania inazalisha umeme wa kutosha ambao ni Takribani Megawati 3796.

Amefafanua kuwa hatua hii ina faida kwa pande zote mbili kwa kuwa njia itakayotumiwa kununua umeme nchini Ethiopia ndio hiyo itakayotumiwa kuuza umeme kwa nchi zenye Uhitaji.

Akifafanunua zaidi amesema kuwa jinsi umeme utakavyokuwa ukinunuliwa, umeme wa Ethiopia utaingizwa kwenye mfumo wa Gridi ya Kenya na kisha Kenya itatoa umeme kuja Tanzania ikifidia umeme ulioingizwa kutoka nchini Ethiopia.

‘’Makubaliano haya yako ya pande mbili kuna wakati sisi tutanunua umeme na kuna wakati tutatumia njia hiyo hiyo kuuza umeme kwa nchi jirani, tunavyoangalia hali ya Kaskazini kwa sasa tunaona sisi tutachukua zaidi kuliko kupeleka lakini kuna wakati na wenyewe wanaweza wakahitaji umeme na tutatumia njia hiyo hiyo kuwapelekea”

Ameongeza kuwa kununua na kuuziana umeme kwa nchi si jambo geni na Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikinunua umeme nchini Uganda kwa ajili ya Mkoa wa Kagera, nchini Zambia kwa ajili ya Mkoa wa Rukwa na nchini Kenya kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tanga hususani ya mpakani.

Aidha, amesema kuwa Tanzania inaendelea na ujenzi wa njia ya Kusafirisha umeme kutoka Tanzania Kwenda Zambia, ambapo kukamilika kwa Mradi huo kutatoa fursa kwa Tanzania kuuza umeme kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

Kuhusu Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere ambalo mpaka sasa limefikia asilimia 99.8 kukamilika amesema limekua na mchango mkubwa wa upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.

“Kule Julius Nyerere sasa hivi tunatumia umeme tunaouhitaji, kama mahitaji yetu sisi ni Megawati 1908 kwenye Gridi ya Taifa hatuwezi kuzalisha zaidi kwa kuwa umeme utakua hauna matumizi”

Pamoja na hayo Mha Mramba ameeleza kuwa Tanzania imejiunga katika masoko ya Pamoja ya kuuziana umeme ya Ukanda wa Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool-EAPP) na Kusini mwa Afrika (Southern African Power Pool-SAPP) ambapo kwa upande wa Kusini mwa Afrika soko lilishaazishwa na linafanya kazi kwa nchi ambazo tayari miundombinu ilishakamilika na kwa sasa Tanzania inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa TAZA ambao kukamilika kwake kutaifanya Tanzania kutumia fursa ya umeme wa unaozalishwa kwenye Bwawa la Julius Nyerere na vyanzo vingine na kuanza kuuza umeme ukanda wa kusini mwa Africa (SAPP).

Hivyo lengo kuu la kuuza au kununua umeme ni kuimarishwa kwa mifumo ya Gridi za Umeme za nchi husika pamoja na kupunguza gharama.Kwa kuzingatia jiografia ya Tanzania itatumia nafasi ya masoko haya ya umeme kununua na kuuza umeme kutoka ukanda wa Mashariki na kusini mwa Afrika.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati inaendelea kuhakikisha kunakuwepo na miundombinu imara itakayowezesha manunuzi na mauziano ya umeme ndani ya ukanda wa EAPP pamoja na ukanda wa SAPP ili Tanzania inufaike kwa kuuza na kununua umeme lakini pia kuingiza fedha zitokanazo na gharama za kupitishia umeme kutoka ukanda mmoja kwenda mwingine.

Wakati Miradi mbalimbali ikiendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa, kuingiza umeme Ukanda wa Kaskazini kuna faida kubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwenye mikoa