Papa Francis, ambaye amekuwa akiugua homa ya mapafu na mkamba kwa zaidi ya wiki tatu, aliwasifu wahudumu wa afya wanaomhudumia kwa uangalizi wao wa huruma.
Kwa Jumapili ya nne mfululizo, papa wa Argentina hakuwepo kutoa baraka zake za kila wiki, lakini Vatican ilishiriki maandishi yaliyotayarishwa na papa.
“Nikiwa hapa, ninafikiria watu wengi ambao wako karibu na wagonjwa,” Papa alisema, akimaanisha wafanyakazi wa matibabu, akiwaelezea kama watu wenye “kuleta mwanga kidogo katika usiku wa maumivu.”
Vatican ilisema Jumamosi kwamba papa ameonyesha “mwitikio mzuri” katika siku za hivi karibuni kkatika matibabu yake yanayoendelea katika Hospitali ya Gemelli ya Roma.
Francis aliandika kwamba anahisi “kutunzwa kwa busara na huruma, hasa kutoka kwa madaktari na wafanyakazi wa afya, ambao ninawashukuru kutoka moyoni mwangu.”
“Nafikiria watu wengi walio karibu na wagonjwa kwa njia mbalimbali, ambao ni ishara ya kuwapo kwa Bwana,” aliongeza.
“Tunahitaji huu – muujiza wa wema – ambao wale walio katika dhiki wanauhitaji, na ambao huleta mwanga mdogo katika usiku wa maumivu,” aliongeza.
