Takriban watu wanane wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi ya usiku yaliyofanywa na Urusi kote nchini Ukraine. Haya ndio tunayojua kufikia sasa:
- Watu wanne waliuawa baada ya kombora la Urusi kushambulia hoteli moja huko Kryvyi Rih, mji alikozaliwa Rais Zelensky katikati mwa Ukraine. Zelensky anasema wafanyakazi wa kujitolea wa Marekani na Uingereza walikuwa wameingia muda mfupi kabla ya shambulizi hilo, na kuongeza kuwa walifanikiwa kutoroka.
- Miundombinu ya raia na uhandisi katika mji wa kusini wa bandari ya Odesa “ilishambuliwa sana” na watu wawili walijeruhiwa, kulingana na gavana wa mkoa huo
- Raia mmoja aliuawa na watu wengine watatu walijeruhi mkoa wa Donetsk, kulingana na maafisa wa Ukraine
- Katika mji wa kaskazini-mashariki wa Ukraine wa Sumy, raia mwingine alikufa baada ya shambulizi la Urusi
- Gavana wa Kharkiv anasema makombora ya Urusi yaliteketeza nyumba na gari na kumuua mtu mmoja
- Wakati huo huo, huko Kherson , mtu mmoja amekufa katika kipindi cha saa 24 zilizopita kufuatia shambulio la Urusi
- Kwa pamoja, Jeshi la Wanahewa la Ukraine limesema lilifyatua mashambulizi 68 kati ya 112 ya ndege zisizo na rubani za Urusi usiku
