Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 05, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kidunga litakalokuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 190

Ujenzi wa Bwawa hilo ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 335.8 ikiwa ni fedha za ndani umefikia asilimia 28 za utekelezaji.

Lengo la mradi huo ni kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji kwa muda wote katika mto Ruvu na hivyo kufanya uwepo wa maji ya uhakika kwa jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na Morogoro.

Vilevile, mradi huo unatarajiwa kuwa na mtambo wa uzalishaji umeme megawati 20, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 101 kutoka Kidunda hadi Chalinze kwenye gridi ya Taifa pamoja na ujenzi wa barabara kiwango cha Changarawe yenye urefu wa kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi Kidunda.

Mradi huo utakapokamilika unatarajia Kuboresha huduma ya Majisafi kwa ajili ya matumizi ya Majumbani, Kilimo na Viwanda kwa kuhakikisha upatikanaji wa muda wote katika mto Ruvu kwa kutiririsha wastani wa lita 24,000 kwa sekunde zitakazokidhi mahitaji ya maji hususani kwenye kipindi cha ukame.