Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema uchaguzi mkuu mwaka huu utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kwani mabadiliko yameshafanyika, hivyo hakuna atakayezuia uchaguzi.

Makalla alieleza hayo leo wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa chama na jumuiya ngazi ya shina, tawi, kata na wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.

“Uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa katiba kwa mujibu wa sheria, nimeona kwenye ‘magroup’ yao wanaambiana wachangiane tone kwa tone tuchangiane tuende kwenye nguvu ya umma kuzuia uchaguzi, hela zitaliwa kwa sababu uchaguzi utafanyika,” alisema Makalla.

Makalla ameongeza kuwa kama watabaki na msimamo wao wa kutoshiri uchaguzi ni dhahiri baada ya uchaguzi mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakitokuwa na nguvu ya kuendelea kuwa chama kikuu cha upinzani nchini, kwani kwa kufanya hivyo kitaua ndoto za wengi wenye ndoto za kugombea udiwani, ubunge na viti maalumu kwani uongozi mpya utakuwa umefifisha ndoto zao.

“Kwa hiyo ambacho ilikuwa inashiriki uchaguzi kilichokuwa kikipata wabunge na madiwani kupitia ndugu yangu anakwenda kuweka alama ya kwamba Chadema inakwenda kufutika kuwa sio chama cha upinzani kikubwa hapa Tanzania,” amesema Makalla.

Aidha, CPA Makalla amesema kuwa ingekuwa ni busara na bora wangesema washiriki uchaguzi na baada ya hapo wakae na kukubaliana ili kufanya mabadiliko.

Rais Samia Suluhu Hassan aliposikia hoja hizi za kufanyika mabadiliko ya uvhaguzi kutoka kwa wadau mbalimbali aliunda kikosi kazi kwa ajili ya kukusanya maoni na kutoa ushauri juu ya sheria zilizopi na akamteua prof Mkandara kuwa mwenyekiti wa kikosi hicho ili kuweza kufanya mabadiliko.

Ameongeza kuwa viliitwa vyama vyote kukutana na kutoa maoni na vyote vilishiriki isipokuwa Chadema kwani walisema walitaka kusikilizwa wakiwa peke yao na walimfata aalitekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana walikabidhi taarifa kwa Mheshimiwa Rais na bila kusita uliandaliwa muswada wa sheria na kupelekwa bungeni.