Na Dotto Kwilasa,JamhuriMediaDodoma
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)imesema kwa kutumia falsafa ya 4Rs (Reforms, Rebuilding, Reconciliation na Resilience,), imepanua huduma za kibingwa kutoka 14 hadi 20 na huduma za ubingwa wa juu kutoka 7 hadi 16.
Hayo yameelezwa leo Machi 4,2025 Jijini hapa na Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel N. Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mafanikio na Mwelekeo wa Hospitali hiyo ukiwa ni Mafanikio ya Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amezitaja huduma hizo za ubingwa wa juu ni Upandikizaji figo kuwa ni pamoja na upandikizaji uloto,upasuaji wa mishipa ya damu , upasuaji wa Moyo kwa kufungua kifua, uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia mawimbi,upandikizaji uume,upasuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu (neuro and spine surgery).

Nyingine ni upasuaji wa uti wa mgongo , kubadilisha nyonga na magoti ,upasuaji wa matundu madogo, Matibabu ya mfumo wa chakula , Matibabu ya magonjwa ya figo, uchujaji damu, Matibabu ya magonjwa ya Moyo,uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo kupitia maabara ya uchunguzi ,uchunguzi na matibabu ya kiradiolojia na Tiba ya Magonjwa ya Hormone na kisukari ,upandikizaji Mimba (IVF) na kuimarishwa na kuboreshwa kwa Huduma za Upandikizaji Figo.
Amesema BMH imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 25 kati ya 50 kwa ndani ya miaka minne kwa gharama ya milioni 875, kati ya hao wagonjwa 10 wamelipiwa matibabu haya kupitia mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiasi cha shilingi milioni 350.
Mbali na hayo amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa sasa ina jumla ya Watumishi 967 kati yao Madaktari Bingwa 81, Madaktari Bingwa wa juu 16, Madaktari wakawaida 65 na Wauguzi 412.
” Hospitali yetu ina Vitanda 400 na kwa siku Hospitali inahudumia wagonjwa wanje 1000 – 1200 na wastani wa wagonjwa 250 hadi 300 wanalazwa. Katika kipindi cha miaka minne, jumla ya wagonjwa 972,740 wamehudumiwa, kufanyika uchunguzi wa vipimo vya kimaabara 1,260,175 na radiolojia ni 272,660,”amesema.
Akieleza Mafanikio Uboreshaji na Kuongeza Huduma zaTiba za Kibingwa na Ubingwa wa Juu amesema BMH ikishirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) zimekuwa zikitoa na kupanua huduma za tiba za kibingwa na Ubingwa wa juu wa Tiba na upasuaji kwa Wananchi mbalimbali wapatao million 14 kutoka mikoa zaidi ya 7 ya Tanzania.

Amesema endapo wagonjwa hao wangekwenda kufanyiwa huduma hiyo nje ya Nchi Serikali ingetumia Shilingi Bilioni 1.875, hivyo kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kimeokolewa. Aidha, uvunaji wa figo UMEBORESHWA kwa Teknolojia ya Kisasa kwa kutumia matundu madogo (Laparoscopic Nephrectomy) ambao ulianza kutolewa Mwezi Novemba 2024 ya chini ya Serikali ya Mheshimiwa Rais Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tangia kuanza, BMH imechangia kupunguza rufaa nje kwa 99%.
Prf. Makubi pia ameeleza kuhusu kuboresha na kuongeza huduma za uchunguzi wa kibingwa kuwa huduma hizo zimeendelea kutolewa ambapo wagonjwa 20,050 wamefanyiwa CT-Scan, wagonjwa 18,456 wamefanywa MRI, wagonjwa 99, 532 wamefanyiwa X-Ray, na wagonjwa 134,622 wamefanyiwa Utrasound.
Katika huduma za maabara kwa kipindi cha miaka minne amesema jumla ya wagonjwa milioni 1.26 walipatiwa huduma ya vipimo vya uchunguzi vilevile vipimo 12,016 vya uchunguzi vilifanyika ili kubaini magonjwa ya kansa kwa njia ya Histopatholojia.
“Pia vipimo vipya vimeanzisha ikiwemo Immunohistochemistry kwa ajili kutambua vimelea vya Kansa, Telepathology, Vipimo vya immunolojia, Vipimo vya Homoni na EEG kwa ajili ya Wagonjwa wenye kifaa ambapo Wananchi 455 wamehudumiwa.
Aidha, katika kipindi hiki maabara yetu mwaka jana ilifanikiwa tena kudumisha ithibati ya ubora inayotambulika inayotambulika shirika la SADCAS, “ameeleza.

Katika kuongeza Upatikanaji wa Dawa na Vifaa tibia amesema BMH imefanikiwa kuongeza upatianaji dawa na vifaa tiba Kutoka asilimia 68 mwaka 2022 hadi 96 kutokana na kuongezwa kwa bajeti yad awa na vituo vya dawa na duka la dawa Jamii
Amesema Hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa ikitoa huduma Mkoba katika mikoa 7 ya Kanda ya Kati na Mikoa ya nje ya Kanda ya Kati ili kuwafikia Wananchi 18,000 wenye uhitaji na pia kuwajengea uwezo watuimishi katika maeneo hayo.
Vilevile imeanzisha huduma mkoba maalumu kwa kutumia magari tembezi yenye vyumba vya upasuaji ambapo huduma hii imeanza kutolewa Zanzibar, kondoa na sasa tunatarajia kwenda Burundi.
Mkurugenzi huyo Myendaji pia ameeleza kuwa Hospital hiyo imefanikiwa kuanzisha miradi ya mkakati ya Miumdombinu ya kutolea huduma za Ubingwa wa juu kwa upanuzi wa huduma za upandikizaji figo kwa thamani ya bilioni 3.7,ambapo itaongeza operation kwa wastani wa 4 kwa mwezi kutoka 2,kuanza kwa Ujenzi wa Kituo cha Matibabu ya Kansa wenye thamani ya bilioni 30.8 ambao utasogeza huduma kwa Wanachi mil 14 na kupunguza rufaa Kwenda Dar es salaam au nje ya nchi Kuongeza vyumba vya Upasuaji.
“Hospitali imefanikiwa kuongeza vyumba vya upasuaji vitatu vyenye thamani ya milioni 250, utasaidia kufanyika operation 50 kwa siku kutoka 30. Hatua hii itapunguza muda wa wagonjwa wetu kusubiri kufanyiwa upasuaji
Kusimika Mtambo wa Kuzalisha Hewa tiba wenye thamani ya bilioni 1.5,”amesema na kuongea;
Mtambo huu unauwezo wa kuzalisha mitungi 400 ndani ya masaa 24, hivyo tumekuwa ukiokoa gharama million 76 kwa mwezi na kuhumia Hospitali za jirani .
“Katika kipindi hiki cha miaka minne Hospitali imeanzisha chuo cha Afya na sayansi shirikishi kwa ngazi ya Stashahada ni chuo cha kwanza kutumia mtaala chini ya NACTVET kwa kozi ya radiographia na uchunguzi wa magonjwa hapa nchini,chuo hiki kinatoa mafunzo ya Utoaji dawa na ganzi, ultrasound katika ngazi ya Astashahada kwa watumishi, “amesema.
Katika eneo la utafiti Hospitali amesema Hospitali hiyo imeendelea kufanya utafiti na kuchapisha katika majarida ya kimataifa ikiwemo kupanua diplomasia ya afya na Taasisi za ndani na nje ya nchi.
“Katika eneo la mashirikiano Hospitali imekuwa na mashirikiano ya wadau wa ndani UDOM, Muhimbili, KCMC, na Bugando na wadau kutoka nje ya nchi kwaajili ya kuwajengea uwezo wataalamu wetu Tokushukai Medical Group – Japan atika kujenga uweoz wa upadikiazaji figo , Help 3 Monza –Italy-kujenha uwezo wa kupandika uloto, Pathology Without Boarder – Italy, Childrens Heart Charity Association – Kuwait, Zgt-Overzee Foundation – Netherland, “ameeleza Prf. Makubi.

Prf.Makubi pia ametumia nafasi hiyo kueleza mwelekeo wa Hospitali hiyo kuwa ni kupandisha hadhi Hospitali kufikia Kiwango cha Hospitali ya Taifa Kuimarisha Mifumo ya TEHAMA katika kuboresha huduma ikiwepo matumizi ya AI katika huduma za kusaidia Wauguzi, customer care , robotic surgeries, upasuaji wa matundu Kukamilisha Miradi ya Mkakati ya Mindombinu inayoendelea
Kujenga vituo vya umahiri vya Upandikizaji Figo (Japan), Uloto (EAC), Upasuaji wa Moyo, Upasuaji Ubongo, ENT , Mama na Mtoto na Tiba ya Macho Ujenzi wa Hostel ya Wagonjwa na Wageni .