Wakazi wa kijiji cha Navikole kata ya Chawi, Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara, wameipongeza serikali kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kijiji hicho ikiwemo umeme, zahanati na maji.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika kijiji hicho cha Navikole, ofisa mtendaji wa ijiji hicho, Turamu Jaha amesema uwepo wa miradi hiyo kijiji hapo kunapelekea wakazi hao kufanya shughuli zao za maendeleo pamoja na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma hizo.

Mkutano huo umeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenda kwa wananchi na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao na kuzifanyia kazi.

Hata hivyo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwenye halmashauri hiyo.

Ofisa mtendaji huyo amesema kufuatia uwekezaji huo uliyofanywa na serikali kijijini hapo na kutolea mfano umeme wananchi wanaendelea na shughuli za kijiingizia kipato kwasababu baadhi yao wanauza vinywaji vya baridi kama vile juisi maji na vingine.

Mkazi kijijini hapo, Juma Ismail amesema kwa sasa kijiji chao kimekuwa na maendeleo makubwa kwasababu huduma muhimu zinapatikana kijijini hapo kama vile huduma ya afya ikilinganishwa na hapo awali.

Aidha kabla ya ujenzi wa mradi wa zahanati kijijini hapo wakazi hao walikuwa wakipata huduma hiyo ya afya vijiji jirani kama vile Chawi ambapo ni takribani kilometa 9 kutoka kijijini hapo, mbawala, kilombero na vingine.

Mkazi mwingine ni Said Salum ameushukuru uongozi wa halmashauri na serikali kwa ujumla kwa uwekezaji huo, “Tunaishukuru serikali kwa kutuletea maendeleo haya hapa kijijini kwetu”

Kwa Upande wake Mbunge wa jimbo hilo, amewataka wakazi hao kuitunza miundombinu ya miradi hiyo ili iwe endelelevu kwa kizazi cha sasa na baadaye.