Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tanga

Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta amesema barabara ya Bagamoyo Mukurunge Pangani- Saadani na Tanga iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Samia Suluhu Hassan ina jumla wa kilomita 256 ikiwa ni pamoja na Daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525.

Amesema barabara hiyo ni sehemu ya barabara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayounganisha Tanzania na Kenya katika Ukanda wa Pwani ya Mashariki amabapo utekelezaji wake unafadhaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Serikali.

Akifafanua juu ya utekelezaji wake amesema mradi huo utekelezaji wake umegawinyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa Barabara ya Tanga –Pangani kilomita 50 yenye gharama ya Sh bilioni 118.7, ambayo utekelezaji wake umefikia asilimia 75.

Sehemu ya pili ni ujenzi wa Daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 amabalo linalogharimu Sh bilioni 107 na kwasasa limefikia asilimai 53.

Sehemu ya tatu ni ujenzi wa barabara ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange yenye kilomita 95 ikujuimisha pia barabara unganishi za Kikungwi inayogharimu kiasi cha bilioni 123 ikijumisha gharama za usimamizi huku ujenzi wake ukiwa umefikia asilimia 46.

Sehemu ya nne ni ujenzi wa barabra ya Mkurunge- Mukange kilomi 73 na mazungumzo yanaendelea.

Akizungumza katika hafla hiyo , Mbunge wa Jimbo la Pangani amabaye pia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ujenzi wa barabra hiyo ni utatuzi wa jambo lilowatesa muda mrefu .

“ Moja ya chanagmoto kubwa iliyotutesa kwa muda mrefu watu wakikata tama, wazee wetu walikuwa waliwahi kusema hivi sisi kwenye mikutano yao hivi sisi kama viongozi tukatufa bila kuona barabara ya Tanga- Pangani Saaadni Bagamoyo?, Nataka niseme Mheshiwa , jambo amablo umelifanya mheshiwa Rais umetotoa Pangoni tunakwenda kupaa angani kwa uchumi na maendeleo” amesema.

Aidha amesema ujenzi wa barabara hiyo utafungua uchumi kwa wnachi, na kuvutia wawekezaji amabao watotoa ajira kwa vijana.

“Pangani ilikuwa kama kisiwa ili mtu aje panagani lazima aje kwa makusudio maalumu, aidha kuziak ama mechi za Simba za Yanaga lakini ujenzi wa barabara hii unakwenda kutufanya kuwa matajari katika maendeleo ya wilaya yetu ya Pangani, na kuvutia wawekezaji’ amesisitiza.