Na Lookman Miraji

Serikali ya India kupitia balozi wake nchini Bishwadip Dey imechangia Dola billioni 1.1 kusaidia upatikanaji wa maji katika miji 28.

Mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya India umelenga kusaidia upatikanaji wa maji safi ya kunywa kwa wakazi takribani 180,000 wa eneo la Korogwe jijini Tanga.

Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la msingi la mradi huo muhimu imefanyika leo hii Handeni mkoani Tanga na kuongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni muendelezo wa serikali ya India kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali nchini.