Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis yuko katika hali mbaya ya kiafya baada ya vipimo vya damu kuonyesha dalili za mapema za kushindwa kwa figo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis yuko katika hali mbaya ya kiafya baada ya vipimo vya damu kuonyesha dalili za mapema za kushindwa kwa figo japo anaendelea kuwa macho na mwenye mwelekeo mzuri.

Taarifa ya Vatican imesema kiongozi huyo wa kidini mwenye umri wa miaka 88 hakupata matatizo zaidi ya kupumua tangu Jumamosi usiku ingawa bado anapatiwa oksijeni kwa kiwango cha juu. Papa Francis anatibiwa homa ya mapafu

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, vipimo vingine vya damu vimeonyesha dalili za awali za kushindwa kwa figo lakini madaktari wamesema hali hiyo inadhibitiwa.

Hali yake ya afya imechochea kufanyika maombi maalum katika makanisa mbalimbali duniani kote kwa ajili ya kumuombea afya njema.