Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimetangaza kutoshirikiana na chama chochote kile cha siasa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 na kusisitiza kusimama wenyewe kwenyek kumpata Rais, wabunge na madiwani.

Chama hicho mwaka 2015 waliungana na umoja wa vyama vya upinzani UKAWA wakakubaliana baadhi ya majimbo waachiwe wakagombee lakini cha kushangaza ,CHADEMA na CUF walipeleka wawakilishi kwenye majimbo hayo wakati huo ni kinyume na makubaliano yao.

Akiongea na waandishi wa habari Februari 18,2025 Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Haji Ambar Khamis amesema kwamba umoja huo hauna tija kwenye chama chao isipokuwa wanaishia kupata maumivu tu

“Sisis tulipitia wakati mgumu sana ,tulikuwa na wagombea wanne wa nafasi ya ubunge,aliyepata ni nafasi moja tu ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia ,kitu ambacho walikosa nguvu kabisa na na walipoteza fedha kupitia umoja huo”,

Adha,amesema kwamba kuna matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa siasa akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia (CHADEMA) Tundu Lisu akisema kutoshiriki Uchahuzi Mkuu ,hivyo hawatahusika na chochote na hawatakubaliana na kauli zake ama matamko anayotoa mara kwa mara kwani wanatambua tunu ya Taifa ya amani alioiacha Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.