Ujumbe wa makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti umetoa wito wa kusitishwa mapigano mjini Goma wakati wa ziara ya viongozi wa waasi waliouteka mji huo mashariki mwa DRC.
Askofu wa Kanisa Katoliki Donatien Nshole amesema makanisa yote mawili yameanza juhudi za upatanishi kati ya waasi na serikali.
“Ziara yetu inalenga kuhimiza mazungumzo, kusikiliza wasiwasi, na kuongeza ufahamu juu ya haja ya haraka ya suluhisho la amani kumaliza mgogoro,” alisema.
“Tunaamini kwamba AFC/M23 inaweza kuchukua jukumu muhimu katika mchakato huu wa kujenga amani,” aliongeza.
Corneille Nangaa, mratibu wa Alliance Congo River (AFC), kundi ambalo linajumuisha M23, aliwakaribisha wajumbe wa kanisa lakini hakutoa maoni yoyote kuhusu majadiliano yao.
Wiki iliyopita, viongozi hao walikutana na rais wa Congo Felix Tshisekedi, na kutoa wito wa kusitishwa mapigano na suluhisho la kisiasa ili kutatua mzozo huo mashariki mwa nchi hiyo.
Kanisa Katoliki lina historia ndefu ya kukuza demokrasia na amani katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ambayo imekumbwa na machafuko katika eneo la mashariki lenye.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002499006.webp)