Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha
Serikali imeombwa kuwapeleka wataalamu katika chuo kikuu cha Dodoma ili waweze kupata mafunzo ya ubobezi katika fani ya TEHAMA ili kuweza kuboresha utendaji kazi wao na kuleta tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Taaluma,Utafiti na ushauri elekezi kutoka Kikuu kikuu cha Dodoma Prof.Razack Lokina wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002497922.jpg)
Amesema kuwa ,kutokana na kamisheni ya TEHAMA kuwa katika chuo hicho na kuweza kufaya vizuri katika TEHAMA ni vyema serikali ikapeleka wataalumu wake kwenye chuo hicho nili waweze kupatiwa mafunzo ya muda mrefu an muda mfupi ambayo yatawapa ubobezi kwenye utendaji kazi.
Ameongeza kuwa, chuo hicho kimekuwa kikifuata maelekezo ya serikali katika kuhakikisha inawekeza zaidi kwenye maswala ya TEHAMA ili kuwezesha shughuli za kitaaluma na kitafiti hali ambayo imeleta mafanikio makubwa serikalini.
“‘Kutokana na jitihada hizo zote tunazofanya tumeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa watalaamu mbalimbali na wanafunzi ambao wamefanikiwa kupita kwenye chuo chetu na wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali’amesema Prof.Lokina.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002497924.jpg)
Naye Mhadhiri wa chuo hicho Ndaki ya Sayansi za Kompyuta na Elimu Angavu ,Salim Diwani amesema kuwa ,wao kama chuo wamefanikiwa kubuni application ya akilli bandia kwa matatizo ya uzazi na hatua za afya ya mtoto .
Salim amesema kuwa ,application hiyo imetengenezwa kwa lengo la kusaidia wamama wajawazito kutatua changamoto watakazokuja kukutana nazo kulingana na hali ya kiafya waliyonayo wakati huo.
Diwani amesema kuwa,utofuati kati ya application hiyo na zingine ni kuwa zile zinatoa ushauri tu wa kitaalamu ila hizi zinatoa utabiri wa kiafya wa changamoto ambazo unaweza kukutana nazo mbeleni kulingana na vipimo vyako vya sasa.
“Kifaa hiki anatumia daktari kuingiza taarifa ya ugonjwa inayoelezea kuwa atapata shida gani ambapo kifaa hiki kinategemewa pia sehemu za vijijini na kitasaidia sana kwani kuna wataalamu wachache sana na wengi wao hawana uzoefu kuhusu maswala hayo.”amesema .
Aidha Diwani amefafanua kuwa,matumizi ya application hiyo itasaidia pia kupunguza foleni ya wagonjwa mahospitalini kwani inaenda kumsaidia daktari katika maswala ya kiafya .
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/1002497925-791x1024.jpg)