Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, amewaagiza wadau wa usalama barabarani kudhibiti ajali za barabarani ambazo zinachangia kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Akijibu swali bungeni mjini Dodoma kuhusu usafiri wa bodaboda, Naibu Waziri Sillo alisema inasikitisha kuona madereva wengi wa bodaboda wakivunja sheria za usalama barabarani licha ya kuwepo kwa mamlaka husika za kudhibiti hali hiyo.
“Tusikubali kupanda pikipiki ya mtu zaidi ya mmoja, kila mtu achukue tahadhari sana,” alisema Naibu Waziri Sillo.
Aidha, Sillo amziagiza mamlaka husika za usalama barabarani kuendelea kudhibiti ajali na kuelimisha umma ili waweze kujilinda, kwa maslahi ya taifa.
![](https://www.jamhurimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/image-33-1024x576.png)