Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko akikaribishwa nchini India na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta na Gesi India, Sandeep Jain mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Indira Gandhi katika Jiji la New Delhi kwa ajili ya kushiriki mikutano mbalimbali ya kimataifa kuhusu nishati.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (kulia) akiwa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Indira Gandhi, jijini New Delhi nchini India kwa ajili ya kuhudhuria mikutano mbalimbali ya kimataifa kuhusu nishati.